Tenzi za Rohoni No 126 - Ni Mji Mzuri
PianoPio PianoPio
23.8K subscribers
1,317 views
0

 Published On Apr 13, 2023

Lyrics: Ni Mji mzuri

1. Ni mji mzuri,
Mbali sana;
Watu wanawiri
Kama jua;
Waimba kwa tamu,
Tuna wema hakimu:
Sifa na idumu,
Kwake Bwana.

2. Ni mji mzuri
Twende sote!
Una na fahari
Msikawe!
Raha tutaona,
Dhambi hapana tena;
Hatutaachana
Siku zote.

3. Ni mji mzuri;
Macho yote
Huko wanawiri
Kama pete;
Baba tutamwona,
Tukifanywa tu wana;
Tumo kupendana
Naye sote.

4. Ni mji mzuri;
Tusipotee
Na tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze, tutume
Kwa taji na ufalme:
Sifa na zivume
Siku zote

Tenzi za rohoni, Wimbo wa tenzi, hymn songs
Tenzi za Rohoni No 126 - Ni Mji Mzuri

show more

Share/Embed