Juma Nature - Mtoto Iddi (Visualizer)
Bongo Records Ltd Bongo Records Ltd
27.8K subscribers
110,423 views
4.1K

 Published On Premiered Sep 26, 2024

LYRICS

Mtoto Iddi kazua balaa

Kijana Iddi kazua mikosi

Mtoto Iddi kazua balaa

Kijana Iddi kazua mikosi

Yuko kama kapandwa na kichaaa

Anahitaji kurekebishwa

Yuko kama kapandwa na kichaaa

Anahitaji kurekebishwa

Kuvumilia Iddi anavyofanya

Inategemea mtu na mtu

Kabila ama kabila

Kuna wengine hawana masihara

Watamletea matatizo asijue wapi pakukimbilia

Watakuletea matatizo usijue wapi pakukimbilia

Iddi zake michapo na pamba za kuazima

Nyumbani ye hakai wanaishi ka makima

Wazazi waliomzaa Iddi anawakosea heshima

Akirudi nyumbani Iddi ananukia pombe

Akiulizwa ametoka wapi anasema dingi usikonde

Na kabla hajaondoka anamkata dingi makonde

Anavyofanya Iddi amerithi kwa baba yake

Sa umleavyo Iddi baba hivyo sio

Atakuja kukamatwa na kesi za mauaji

Iddi ukimtazama ni mtoto wa makamo

Vibaka wamekamatwa ye mwenyewe akiwemo

Wamemfikisha kwa baba yake kasema simo

Wamempiga mapanga kujifanya much know

Anaunguruma na kesi ya kumdhulumu Mr Joseph Kusaga

Hivi sasa anatafutwa alilipe lile deni alilokopa kwa bwana Joe

Ana kesi za wizi zipatazo ishirini na sita

Alivyo na bahati mbaya akikwapua tu wanamshika

Wazazi mpaka mwenyewe ndio ****

Amepoteza nafasi ya kuishi kama Soldier

Kwani Iddi hawezi kula ugali bila mboga

Kutwa nzima Iddi anakaa kizembe wamemroga

Na tena kuna tetesi wanga wamekula kiboga

We Iddi kuwa makini tabia yako haifai

Utapondwa na marungu uone dunia ka hafai

We ni shahidi ni shahidi

Mtoto Iddi kazua balaa

Kijana Iddi kazua mikosi

Mtoto Iddi kazua balaa

Kijana Iddi kazua mikosi

Yuko kama kapandwa na kichaaa

Anahitaji kurekebishwa

Yuko kama kapandwa na kichaaa

Anahitaji kurekebishwa

Kuvumilia Iddi anavyofanya

Inategemea mtu na mtu

Kabila ama kabila

Kuna wengine hawana masihara

Watamletea matatizo asijue wapi pakukimbilia

Watakuletea matatizo usijue wapi pakukimbilia

Iddi ni kijana mwenye sura ya kibandidu

Iddi ni mtoto wa kwanza wa mzee Hamidu

Ukisema tumseme we ni kama umemuadhibu

Huyu Iddi ana laana

Kutumwa kwake ni kama umemuonea

Mkimuachia upenyo mnamkuta amepotea

Haoni raha kuishi ye na yake familia

Katoka na pombe zake tu akirudi ye analia

Anamlilia nani na pombe kanywa mwenyewe

Na huo ni ushauri alioupata kwenye vijiwe

Mzee Hamidu ana dharau kusema lolote liwe

Alianza tu kidogo ye kubadilisha bia

Mtu mzima yupo bar anazitiririsha bia

Anasubiri wateja walewe aweze kuwaibia

Kamatwa kila wiki watu wameshatega njia

Watu wamechukia nini kinachofatia

Ni kumponda na kumuua au Mungu kumuokoa

Huyu Iddi ana laana

Iddi matatani hawezi kupenya dirishani

Wala haishi kwa raha amemuibia na Majani

YeKila siku kesi tu haziishi mahakamani

Asikutane na msamaha

Pita pita kona naona kundi la watu

Wanambeba Iddi kaiba viatu vya watu

Nauliza eti kisa kauza viatu vya watu

Bila mwenyewe kujua kama Iddi amechukua


Song Writer:
Juma Kassim Ally
  / sir_nature  

Audio produced & mixed by:
P-Funk Majani
  / majani187  

Video directed by:
Numz Visualz
  / director_numz  

show more

Share/Embed